NINGETAMANI MANJI NA ''MO'' WAWE WAMILIKI NA SI VIONGOZI.NINGETAMANI MANJI NA "MO" WAWE WAMILIKI NA SI VIONGOZI.

Ligi yetu imefikia ukingoni, na timu ya Yanga imenyakua ubingwa wa ligi hiyo huku Coastal union, African Sports ns Mgambo zote za Tanga zimeshuka kwenda daraja la kwanza. 

Leo nawaza sana nje ya uwanja jinsi gani tunaweza kuendesha vilabu vyetu kwa mafanikio. Naziangalia Simba na Yanga kwa sababu kubwa tatu.

Kwanza ni "brand" kubwa, pili ni vilabu vikongwe na mwisho ndiyo alama ya mpira wetu kwa maana ndiyo waliobeba taswira ya mpira wetu. 

Simba kuna fukuto kati ya viongozi na wanachama kutokana na matokeo mabaya waliyoyapata kwa misimu kadhaa sasa.
Yanga wanakaribia kufanya uchaguzi mwezi ujao, na mwenyekiti wa sasa bwn Yusuph Manji anatarajiwa kugombea na kuitetea nafasi hiyo ktk uchaguzi ujao.
Sina nia ya kujadili suala la vurugu za Simba wala kuingilia mchakato wa uchaguzi wa Yanga kwa namna yoyote.
Najaribu kufikiria njia muafaka ya kuongoza na kuvipa mafanikio vilabu vyetu.
Ungeniuliza njia bora ninayoiota leo ni kuvibinafsisha vilabu hivi viwe biashara za watu, mashabiki na wapenzi tubaki kushangilia na kubishana kijiweni.
Jaribu kufikiria namna Yusuph Manji alivyoituliza klabu na mwenendo wa klabu hiyo ktk ligi huku akiwa mwenyekiti tu ambaye muda wake wa uongozi hukoma.
Endapo Manji angekuwa mmiliki wa klabu namna anavyowekeza ingebadilika, usimamizi wa uwekezaji huo ungebadilika na hata mtazamo wake juu ya uwekezaji huo ungebadilika. Ukimuuliza leo juu ya matumizi yake kwa klabu atakwambia lengo lake ni kuwapa watu furaha. Lakini angekuwa mmiliki lengo lake lingebadilika na kuwa biashara.
Kama Manji na "Mo" wangekuwa wamiliki wa Yanga na Simba ningekuwa na uhakika wa kuwaona wote ktk hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa Africa.
Mjadala juu ya biashara kwa kutumia nembo za klabu ungekufa kifo cha kawaida.
Ukiuliza mtu yeyote mwenye mapenzi mema na Yanga unataka nani aongoze klabu zaidi ya asilimia 70watakuambia Manji, swali ni je! Kwanini basi tusimfanye kuwa mmiliki? Ili tusonge mbele kuelekea kule ambako mpenda soka yeyote anatamani tuelekee.
Ili kufuta ubwenyenye wa baadhi ya watu wanaoamini kuwa Simba haiwezi kufanya vizuri bila wao, njia ni kufanya "Mo" awe mmiliki.
Wapeni kazi wataalamu wa maswala ya uchumi, biashara na hisa wathaminishe tupate utaratibu wa jinsi ya kuziingiza ktk soko la hisa, asilimia 60 ichukuliwe na matajiri hawa na ile 40 iliyobaki tununue sisi wengine ili tupumzike kusikia migogoro isiyo na kichwa wala miguu.
Tuanze kukimbilia maendeleo sasa, kwani siyo sifa kubaki nyuma wakati dunia inakimbia kwenda mbele. 
Imani K Mbaga.
0717469593
Post a Comment
Powered by Blogger.