Ni Vita Ya Mbeya City Na Yanga Leo Huku Azam Yaushikilia Ubingwa Wa Yanga TFF Yakata Rufaa.

Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara kuendelea leo kwa mchezo mmoja kuchezwa mjini Mbeya wenyeji Mbeya City watawaalika wanajangwani Yanga wanahitaji pointi moja ili waweze kutawazwa mabingwa kutokana na klabu ya Azam kukata rufaa kutokana na kupokonywa pointi kwa kumtumia mchezaji mwenye kadi tatu za njano.
Mbeya City.
Mchezo huu unatarajiwa kuwa mkali kwa timu zote mbili ili kuonyesha ufalme kwa mwenzie huku Yanga wanataka kuendeleza Rekodi ya kuifunga Mbeya City kwani tangu ipande ligi kuu haijawahi kuifunga Yanga hata mchezo mmoja.
Yanga.
Klabu ya Yanga kupitia msemaji wake Jerry Murro ametangaza kuwa vita inaendelea na dozi kama kawaida lazima wawafunge wenyeji ili kuendeleza kufanya vizuri kwenye mechi zote zilizo mbele yao.
Azam.
Kwa taarifa zilizoenea ni kuwa klabu ya Azam imekata rufaa kwa TFF kwa mchezaji wao kuwa hakuwa na kadi tatu za njano hii ina maana kuwa watauchelewesha ubingwa wa Yanga na inapelekea leo mechi ya Mbeya kuwa ngumu  kwani Azam wana pointi 60 wakiwa na mechi tatu kama wakishinda watafikisha pointi 69 huku Yanga wana pointi 68 wakiwa nao na mechi tatu hivyo lazima washinde mchezo mmoja ili waweze kutawazwa mabingwa wapya.
Post a Comment
Powered by Blogger.