NI VITA NYINGINE YA HESHIMA JIJINI DAR ES SALAAM LEO.

NI VITA NYINGINE YA HESHIMA JIJINI DAR ES SALAAM LEO.

Bila shaka katika miaka ya karibuni mechi kati ya Yanga na Azam ni moja kati ya michezo ya kusisimua na inayovuta hisia za wapenzi wa soka katika ukanda huu wa Afrika Mashariki.
Ningekuwa natengeneza "odds" za mchezo huu ningewapa Yanga 2. 40, Azam 2. 60 na sare 2. 90.
Kwa kusema hivyo maana yake ni kwamba huu ni mchezo mgumu na usio tabirika.
Nategemea kuona Azam isiyofunguka, eneo la kati ikiwa chini ya wakabaji halisi Mugiraneza, Himidi Mao "mmoja kati ya viungo ninaowahusudu sana" Mudathir akianzia benchi "0kutegemeana na mpango wa mchezo wa mwalimu" .
Ninategemea kumwona Kipre Tcheche aking'ara ktk eneo la ushambuliaji. Aish Manula ni mmoja kati ya walinda mlango wanaoisumbua sana Yanga na yy hung'ara sana katika mechi hii.
Azam hutumia nguvu sana wanapocheza na Yanga, labda kwa sbb ya upinzani uliojengeka kati yao ktk miaka ya karibuni.
Kwa úpande wa màbingwa wa ligi Dar Young Africans, sitegemei kuona mabadiliko makubwa kiuchezaji, ni timu iliyokaa pamoja kwa muda mrefu, na wakiwa na wachezaji waliokonga mioyo ya wapenzi wao katika sehemu ya kiungo Thaban Kamusoko,, katika eneo la ushambuliaji Donald Ngoma na Amis Tambwe nk
Nategemea kuona nguvu kubwa ikitumika eneo la kati ya uwanja na bila shaka Yanga watakuwa bora kati ya uwanja ingawa Azam watakuwa na mbinu nyingi zaidi.
Mechi nyingi kati ya Azam naYanga huwa zinaamuliwa kwa sare na mm nategemea leo mechi iamuliwe ndani ndani ya dkk 90. .
Mwamuzi ni Israel Nkongo sitegemei kama atakuwa nautàtà ktk maàmuzi ña kutúharibia mchezo huu
Tukutane baada ya dkk 90 hapo jioni.


Imani K Mbaga 0717469593
Post a Comment
Powered by Blogger.