Ni Vita Na Kisasi Nusu Fainali Ya Pili UEFA Champions League,Je Bayern Munich Watapindua Matokeo Leo?

Michuano ya Ligi ya mabingwa barani Ulaya kuendelea tena leo katika hatua ya nusu fainali ya pili kuelekea katika hatua ya fainali itakayochezwa nchini Italia.
Bayern Munich.
Katika uwanja wa Arena nchini Ujerumani wenyeji Bayern Munich watawaalika Atletico Madrid mchezo huu utakuwa mgumu na mkali kutokana na mechi ya awali Munich alifungwa bao 1-0 na hivyo wanahitaji kupindua matokeo ili waweze kutinga fainali.
Atletico Madrid.
Huku kocha wa Atletico Madrid Diego Simeone,amemuonya kocha wa Munich kuwa asitegemee mteremko wa kushinda mechi ila na ameahidi kuweka rekodi dhidi ya wenyeji hao na kuweza kutua fainali na hatimaye kuchukua ubingwa wa michuano hiyo.
Wachambuzi wa soka wanadai kuwa Bayern wataweza kutinga fainali kwa kuifunga Atletico Madrid na hatimaye kuchukua ubingwa na kuweza kumuekea rekodi Pep Guardiola.

Post a Comment
Powered by Blogger.