Ndege Ya Misri Yatoweka Angani Ikitokea Paris Nchini Ufaransa.

Ndege moja ya shirika la ndege la Misri la EgyptAir, iliyokuwa ikitoka mji mkuu wa Ufaransa Paris hadi Cairo, imetoweka kutoka kwenye mitambo ya rada.
Maafisa wanaosimamia safari za ndege wanasema kuwa ndege hiyo aina ya Airbus A320, ilikuwa na abiria 59 na wahudumu kumi.
Shirika hilo limesema kuwa ndege hiyo ilitoweka katika maeneo ya mashariki ya bahari ya Mediterranean, kilomita 16 kabla ya kufika katika anga ya Misri.
Hakuna dalili zozote za kuwepo kwa hali mbaya ya anga na Misri imetuma ndege za kivita kusaka ndege hiyo kwa ushirikiano na utawala wa Ugiriki.
Post a Comment
Powered by Blogger.