Wema Sepetu Alilia Mahakamani Kisa Hoteli Huku Akitoa Tamko.Kufuatia kuvuja kwa picha za chumba alicholala na kumtia aibu kutokana na mazingira aliyoyaacha, staa wa sinema za Kibongo, Wema Sepetu ‘Madam’ ameibuka na kuamua kuchukua hatua ya kuushtaki mahakamani uongozi wa Hoteli ya Golden Crest, iliyopo jijini Mwanza. ISHU ILIANZA WIKI ILIYOPITA
 Picha hizo zilisambaa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya mmoja wa wahudumu wa hoteli hiyo kudaiwa kuisambaza video iliyokionesha chumba alichokuwa amelala mrembo huyo kikiwa vululuvululu huku vipisi vya sigara na bangi vikisambaa. “Jamani hichi ndicho chumba alicholala Wema Sepetu, yaani ametufanyia vibaya sana kwa kweli kwa kuacha chumba katika hali hii,” alisikika mtu huyo aliyedhaniwa ni mhudumu. 

 WEMA AZODOLEWA Mara baada ya video hiyo kuzagaa mitandaoni, wafuasi wa mitandao mbalimbali walicharuka kwa kumpa maneno ya ‘shombo’ Wema kwa kutokuwa mstaarabu na kwenda mbali zaidi kwa kusema ni aibu kwa mrembo kama yeye mwenye jina kubwa Bongo, kuacha chumba kikiwa kichafu namna ile. “Ustaarabu ni kitu cha bure jamani. Haiwezekani mtu uingie hotelini halafu ukiache chumba katika hali ile,” alichangia mdau mtandaoni. WENGINE WAMTETEA… Hata hivyo, pamoja na kuwepo na wafausi wengi waliomkosoa Madam kwa kitendo hicho, kuna baadhi ya watu walimtetea wakidai suala la usafi  hupaswa kufanywa na wahudumu kwani ndiyo kazi yao. “Ni jukumu la wahudumu kufanya usafi  kwani Madam si amelipa? Waache kumuonea,”alichangia mdau mwingine. WEMA HUYU HAPA Kufuatia kuzagaa kwa taarifa hizo mitandaoni huku vyombo vingi vya habari vikimsaka Madam kwa muda mrefu ili atoe ufafanuzi bila mafanikio, Risasi Mchanganyiko liliweka ‘fowili’ na kufanikiwa kumpata  Miss Tanzania huyo wa mwaka 2006 ambapo alifunguka kwa kirefu kuhusiana na ishu hiyo na kueleza azma yake ya kuwaburuza wahusika wa hoteli hiyo mahakamani. “Mimi nimeshaanza kuchukua hatua ya kisheria kwa hoteli hiyo, nawafi kisha mahakamani maana naona hawajanitendea haki. Hata wateja wao wataogopa kwenda kama wanakuwa na kazi ya kurekodi vyumba vya wateja wanaokwenda kulala na mbaya zaidi hata walivyoweka vitu vingine si kweli kuwa ndivyo nilivyoacha mimi, wanataka kunichafua tu,” alisema Madam. HOTELINI WANASEMAJE? Gazeti hili lilifanya jitihadi za kuwasiliana na uongozi huo ambapo lilifanikiwa kuzungumza na meneja wa hoteli hiyo aliyejitambulisha kwa jina la Peter Ernest, ambapo alisema hata wao walipata taarifa za kusambaa kwa picha hizo, lakini akadai hotelini kwao hakuna hata mtu mmoja aliyehusika na ishu hiyo. “Sisi wenyewe tulisikia hiyo ishu lakini kutakuwa na mtu ambaye amemfanyia mchezo huo mchafu na si wa hotelini kwetu, kwa sababu hata kama itakuwa ni kutushtaki, sisi hatujui lolote ni watu tu wanataka kuchafua hoteli yetu na kumchafulia Wema,” alisema meneja huyo.
(CHANZO; RISASI JUMATANO/GPL
Post a Comment
Powered by Blogger.