MHADHIRI WA UDSM ANETH MWAKILILI AWA BALOZI WA ALL-STARS STUDENTS AWARDS

Add caption
Mratibu wa Tuzo za wanafunzi bora, michezo na wenye vipaji maalumu wa Afrika Mashariki, Dj Aaron Tanzania amemtambulisha Aneth David Mwakilili Mhadhiri Msaidizi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam, UDSM, Dpt. of Molecular Biology and Biotechnology kuwa balozi wa tuzo hizo.Aneth ni mshindi wa tuzo maarufu za Sayansi duniani inayofahamika kama The Next Einstein Forum (NEF). Arnold Gosbert, Aneth Mwakalili na Dj Aaron Tanzania
 
Ameteuliwa na ASSA2016 kuwa balozi kutokana na umahiri wake kwenye masomo ya sayansi na ushindi alioupata pia na uzalendo alionao kwa nchi yake.

ASSA2016 ni tuzo zitakazotolewa kwa wanafunzi wa shule za Afrika Mashariki.

Tuzo hizo zina dhumuni la kuwapa hamasa wanafunzi wa shule za Afrika Mashariki. Tuzo hizo zitatolewa kwa wanafunzi watakaofanya vizuri kwenye mitihani ya kidato cha nne na sita. Masomo yakayotolewa tuzo ni Kiswahili, Hesabu, Fizikia, Kemia, Bailojia na Kiingereza. Mchakato wa tuzo utaanza katikati ya mwezi wa sita.
Post a Comment
Powered by Blogger.