Matangazo Ya Bidhaa Za Uzazi Wa Mpango Marufuku

 
Mipira Ya Kondomu Bodi inayodhibiti matangazo ya redio na runinga nchini Pakistani imeagiza vituo vya utangazaji kuondoa matangazo hayo kutokana na lawama za raia, kuwa yanawafanya watoto kuwa wenye kutaka kujua sana.
Mwaka jana tangazo la aina moja ya kondomu lilipigwa marufuku kwa madai lilikua na maudhui ya upotoshaji, japo matangazo ya dawa za kupanga uzazi huwa nadra sana katika taifa hilo la kihafidhina.
Pakistan inaorodheshwa ya sita duniani kwa idadi kubwa ya watu.
Umoja wa Mataifa unasema thuluthi moja ya raia wa taifa hilo hawafikiwi na huduma za kupanga uzazi.

Chanzo: BBC
Post a Comment
Powered by Blogger.