Malkia Elizabeth,Asema Maafisa Wa China Ni Wajeuri.

Rais wa China akiwa na Malkia wa Uingereza.
Malkia Elizabeth amenaswa kwenye kamera akisema maafisa wa China ni 'wajeuri sana' wakati wa ziara rasmi mwaka jana ya rais Xi Jinping.Alikuwa akimueleza afisa mkuu wa polisi katika kasri la Buckingham, jinsi balozi wa Uingereza kwa China alivyopokewa.
Matamshi yake yanajiri baada ya waziri mkuu David Cameron kusikika akisema Afghanistan na Nigeria ni mataifa yenye "ufisadi mkubwa". Kasri la Buckingham limesema ziara ya kiongozi huyo wa China "ilikuwa na ufanisi mkubwa".

Mualiko kwa rais Xi ulikuwa sehemu ya sera ya serikali kujaribu kuvutia uwekezaji wa China.
Matamshi ya malkia yalinaswa kwenye kanda wakati akijulishwa kamanda muu wa polisi Lucy D'Orsi, ambaye alifahamishwa ndio aliyesimamia usalama wakati wa ziara ya rais Xi Uingereza mnamo Oktoba.
Anasikika akisema: "Oh, bahati mbaya"
Afisa mmoja aliendelea kumueleza malkia kwamba kamanda D'Orsi "alidharauliwa sana na Wachina lakini alifanikiwa kujizuia na kuendelea kufanya kazi".
Kamanda D'Orsi alimwambia malkia: " mimi ndiye niliyekuwa kamanda mkuu, sijui kama unalifahamu hilo, lakini ulikuwa mtihani mkubwa kwa..."alisema Malkia
Kamanda D'Orsi akaendelea: "ilikuwa ni ule wakati walipotoka Lancaster House na kuniarifu kwamba safari imesitishwa, nilihisi...."
Malkia akasema: "walikuwa wajeuri sana kwa balozi."
D'Orsi akajibu: " ni kweli... Ni ujeuri mkubwa na nilidhani sio jambo la kidiplomasia."
Msemaji wa kasri la Buckingham baadaye alisema: "hatuzungumzii mazungumzo ya faragha ya malkia. "hatahivyo, ziara ya kiongozi wa China ilikuwa na ufanisi mkubwa na pande zote zilishirikiana kuhakikisha iliendelea vyema."
Hakujakua na tamko rasmi kutoka maafisa wa serikali China lakini matangazo yanakaguliwa huku habari na vyombo vya habari zilizimwa ilipoangazia mazungumzo hayo.
Post a Comment
Powered by Blogger.