Magufuli - Askari Alietukanwa Na Mke Wa Waziri Apandishwe Cheo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemuagiza Kamishna wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Ernesti Mangu kumpandisha cheo askari wa Usalama barabarani ambaye alitukanwa na Mke wa Waziri wakati akitekeleza majukumu yake ya kikazi.
 Rais ameyasema hayo wakati akifungua Kikao cha Makamanda wa Polisi wa Mikoa. Aidha Rais Dr. Magufuli amesema ameshamuonya Waziri huo ambaye mke wake amemtukana askari wa Usalama Barabarani.
Wakati akitoa agizo hilo, rais amesema hakuna kiongozi au familia ya kiongozi iliyoko juu ya sheria.

Post a Comment
Powered by Blogger.