Leiceater City Kawa Mwalimu Wa Mbeya City Na Wakili Wa Timu Ndogo,Soma Makala Hii Ya Imani K.Mbaga.

Nembo ya Leicester City.
LEICESTER CITY KAWA MWALIMU WA MBEYA CITY NA WAKILI WA TIMU NDOGO
Dunia ya soka imepigwa butwaa kama siyo kupatwa na mshtuko kuona vijana wa Leicester City wanabakiza alama tatu pekee kuwa mabingwa wa soka nchini England.
Baada ya kurejea ligi kuu msimu uliopita Leicester wakajikuta ktk msimu wao wa kwanza wanaponea chupu chupu kushuka tena ligi daraja la kwanza. Hali hiyo iliwafanya wachambuzi maarufu duniani siyo tu kutoipa nafasi bali kutoifikiria kabisa kwamba Leicester inaweza kuwa angalau ktk nne bora kwa vigezo vyote iwe thamani ya kikosi hadhi ya wachezaji au hata ubora wa matokeo yaliyopita.
Juma hili tunasubiri kuona namna Leicester watakavyozichanga karata zao ktk mechi tatu zilizobaki wakihitaji alama tatu tu kati ya tisa zilizopo mbele yao.
Thamani ya kikosi cha Leicester city kwa wachezaji wote jinsi walivyo nunuliwa ni sawa na thamani ya wachezaji wawili wa Manchester City au wawili wa Arsenal au wachezaji watatu wa Tottenham.
Kikosi hicho kina thamani ya pauni milioni 54.4 hv, ambapo fedha hizo pale Man City zimemnunua Eliaqim Mangala na Fernando, kule Arsenal hizo zimewanunua Ozil na Chamberlain, au pale Totts ndizo zilizotumika kuwanunua Lamella, Ericksen na Dembele.
Tuna mengi ya kujadili kuhusu hiki kilichotokea kwa Leicester msimu huu ambapo hata ikitokea bahati mbaya ya kutonyakua ubingwa watakuwa wameacha historia ya "kuwahenyesha" wakubwa ktk mbio za ubingwa wa England.
Leicester wamenikumbusha hadithi moja tamu ya ujio wa vijana wa Mbeya City. Baada ya msimu wa kwanza kuwakimbiza watu wazima na kuingia ktk nne bora kdg na msimu uliofuatia pia, msimu huu Mbeya City wanashika nafasi ya 10.
Leicester msimu huu wametoa masomo kwa timu ndogo
1. Kutokamia mechi moja hasa zile kubwa tu, maana ukiwatazama Leicester ktk michezo yao yote walicheza kama fainali, hawakuchagua mechi
2. Walikuwa na nidhamu ya hali ya juu! hawakubweteka na mafanikio madogo. Huku ukimfunga Simba au Yanga unainua mabega na kupoteza malengo, hawa jamaa walifungwa na Arsenal tu lkn waliwakimbiza big four wote na bado hawakuridhika
. Hawa Leicester waliyatumikia malengo yao hawakutumikia maléngó ya watu wengine, hawakutumiwa wala kutumikia watu wengine, bali walitumikishwa na malengo yao
3.Walijituma kufikia hapa walipofika, njia pekee ya kushindana na aliyekuzidi ni wewe kufanya kwa kutumia nguvu mara mbili yake "work rate"

Post a Comment
Powered by Blogger.