LADHA MCHANGANYIKO LIGI YA UINGEREZA MSIMU UJAO.


Imani Kelvin Mbaga's photo.

LADHA MCHANGANYIKO EPL MSIMU UJAO:

Gumzo kubwa linaloendelea hivi sasa ni ujio wa Jose Morinho ktk klabu ya Manchester United ya kule nchini Uingereza. 

Morinho akitokea fc Porto hadi Chelsea, baadae Inter Milano hadi Real Madrid na sasa kwa mabingwa wa kihistoria Manchester united.
Morinho rafiki mkubwa wa vyombo vya habari kwa namna anavyojua kutengeneza habari siyo mgeni katika ligi kuu nchini Uingereza


Aliifundisha Chelsea kwa mafanikio makubwa ktk awamu zote huku akiwapa taji la ligi kuu baada ya miaka hamsini hiyo ikiwa msimu wa 2004/2005. 


Habari ya kuja kwa Morinho pale Old trafford ilianza siku nyingi kama tetesi lkn sasa imeshakua kweli.
Jambo linalosisĂ­muĂ  ni kuona ushindani wa kiufundi na kimbinu hapo msimu ujao.
Ninapojaribu kupata taswira ya msimu ujao akilini mwangu nayaona makundi mawili ya waalimu..


KUNDI A "UFUNDI".


››› Pep Guardiola
››› Jurgen Clopp
››› Arsene Wenger.


Hili ni kundi la waalimu wanaopenda ufundi mwingi, na hata usajili wanaoufanya mara nyingi huangukia kwa wachezaji wenye vipaji vya kuchezea mpira huku timu wanazofundisha hucheza kwa kufunguka, kushambulia na migongeo au "pasi" nyingi..
Najaribu kufikiria ile "tik tak ya lamasia"kutoka Barca au Borussia Dortmund ya Klopp ndivyo nitakavyoiangalia mechi kati ya Man City na Liverpool msimu ujao. 


KUNDI B " MBINU"
›› Jose Morinho
›› Antonio Konte
›› Claudio Ranieri
›› Mouricio Pochettino.


Hawa kwangu mimi ni mabingwa ma wataalamu wa mbinu.
Navuta picha picha ya Juve ya Antonio Conte na na ukuta wa Inter ya Morinho ndivyo nitakavyokuwa naangalia mechi kati ya Man U na Chelsea msimu ujao.
Nategemea vita ya ne bora "top four" ikiwa ngumu zaidi msimu ujao pengine kuliko misimu mingine iliyopita.
Nje ya uwanja nafikiria mikutano ya waandishi  wa habari baada ys mechi huku wasemaji wakiwa mzee Arsene Wenger, au Jose Morinho au Klopp.
Haya ni baadhi ya mambo yanayo yanayonifanya niwaze sana juu ya msisimko ujao wa EPL.Imani K Mbaga
0717469593

Post a Comment
Powered by Blogger.