Makala Kuhusu,Kwa Mwendo Huu Tunatengeneza Ligi Ya Timu Mbili?KWA MWENENDO HUU TUNATENGENEZA LIGI YA TIMU MBILI.

Unapokuwa mpenda soka, kila wakati kuna linakujia kichwani na kukufanya utafakari kuhusu mustakabali wa soka iwe ndani au nje ya Tanzania.
Wiki hii nikiwa nafuatilia mambo mbalimbali yanayoendelea ktk soka letu kupitia vyombo vya habari na mijadala mbalimbali inayoendelea kuhusu soka hapa nchini, kwa mbali naanza kuona maandalizi ya ligi ya timu mbili Tanzania. Bahati mbaya sana wanaondaa ligi hiyo ni vilabu na baadae wataanza kumtafuta mchawi wa kumbebesha lawama.
Wakati tunapotaka kuiadabisha TFF na kuinyoosha ili soka letu lisonge mbele ni lazima tuhakikishe tunaziba mianya yote ya udhaifu katika vilabu vyetu ili kutotoa nafasi kwa shirikisho au adui yoyote wa soka letu kutumia udhaifu wa vilabu kujinufaisha na kulididimiza soka letu.
Duniani kote ligi mbalimbali zinafikia mwisho wakati ambapo tayari maandalizi ya msimu ujao tayari yameanza, watu wanazungumzia usajili uboreshaji wa mabenchi ya ufundi na mikakati ya ushindi.
Hapa kwetu nasikia na kuona zogo kwenye vyombo vya habari badala ya kuona mipango na mikakati ya jinsi ya kufanya vzr msimu ujao. Kule Tanga wanachama wanaitaka timu yao, Ndanda baadhi ya wajumbe wa kamati ya utendaji wameanza mzozo juu ya kuhamisha mechi yao dhidi ya Yanga, huko Shinyanga Stand Utd nao wanachama wa asili wanataka uchaguzi na tayari wameanza mzozo, Toto Africa walianza ugomvi muda mrefu, Simba wanachama wanataka timu yao huku uongozi ukihangaika kuwapoza wanachama wao kwa kupambana na Kessy, Hajib na kuizunngumzia mechi ya Yanga na Ndanda ambayo haina faida yyt kwao.
Haya ni baadhi tu ya mambo yanayoendelea ktk vilabu vyetu vitakavyoshiriki ligi msimu ujao na kutaka matokeo bora. Lakini wakati vurugu hizo zinaendelea Yanga wanazungumzia usajili wakati Azam tayari wapo kwenye mazungumzo na kocha mpya ili kubadilisha benchi lao la ufundi. Kumbuka kwamba wakati wengine watakapokuwa wanatulia tayari ligi itakuwa inakaribia kuanza hivyo timu nyingi zitakuwa hazina makocha, usajili utafanyika kwa zimamoto kambi za kubahatisha na mara ligi inaanza.
Kumbuka endapo Yanga itafanikiwa kuingia hatua ya makundi ya kombe la shirikisho barani Africa hiyo itamaanisha kuwa watauanza msimu ujao wakiwa na uzoefu, pamoja kwa muda wa kutosha nk kitu ambacho ili kushindana nao unahitaji utulivu na juhudi kubwa sasa bado najiuliza je? Kwa jinsi klabu zetu zinatengeza mazingira ya maandalizi kwa msimu ujao tutegemee nn?
Nilitegemea hamasa kwa timu za mikoani kuandaa mikakati ya kusaka fedha ili waanze kambi na usajili mapema.
Kwa nn msiandae chakula cha hisani kwenye mikoa yenu na kuwashirikisha wananchi, kutengeneza jezi, kalenda nk ili kupata fedha nje ya udhamini wa Vodacom na Azam yote hii iwasaidie kujiandaa na msimu ujao.
Inawezekana tukawa vipofu sasa tusione haya, lakini siku zote muda unaongea.
Malizeni tofauti zenu jiandaeni mapema kwa ajili ya msimu ujao, ili muwape wapenda soka haki yao. 


 


Post a Comment
Powered by Blogger.