Kwa Mara Ya Kwanza Ni Historia Raia Wa Africa Mashariki Wakutana Zimbabwe Watoa Ujumbe Mzito.

Raia wa Afrika Mashariki wanaoishio Zimbabwe wamefanya mkutano wa kwanza wenye lengo la kushirikiana kwenye nyanja tofauti.
Pamoja na mkutano huo wa Harare, kuwakutanisha kwa mara ya kwanza raia wa nchi zote za Afrika mashariki pia wameitumia siku hii kumkaribisha mwanachama mpya Sudan ya Kusini.
"Sisi ni watoto,hatuwezi kula Ugali na watu wazima, ninachukua nafasi hii kuomba mtulee tukue tuwafikie" Amesema Gabriel Riek Balozi wa Susan Kusini nchini Zimbabwe na kuongeza kuwa Sudan ina fursa nyingi kwa nchi wanachama ikiwamo kuwakaribisha kufundisha Kiswahili kwani nchi hiyo imeanza kusisitiza Lugha ya Afrika Mashariki.
Naye Balozi wa Kenya nchini hapa Bi Lucy Chelimo amesema amefurahishwa sana na na utaratibu huu kwani mara zote kila nchi imekuwa ikifanya matukio yake hali ambayo imekuwa inachelewesha mshikamano.
Aidha Balozi Chelimo ameahidi kuwa nchi zote wanachama ziko tayari kuisaidia Sudan kusini kuimarika.
Kwa upande wake Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe Luteni Jenerali Mstaafu Charles Lawrence Makakala amesema kila mwaka watahakikisha wanawakutanisha wananchi wa afrika mashariki waishio hapa ili kufahamiana na hata kubadilishana taarifa zinazoweza kufungua fursa miongoni mwao.
Wananchi wa nchi zote sita zinazounda jumuiya ya Afrika mashariki waliofika katika tukio hili lililofanyika katika Ubalozi wa zamani wa Tanzania mjini Harare wamesema wamejifunza mengi kwani kila mmoja kuna lililomleta Zimbabwe hivyo wamebadilishana ujuzi na pia watoto wao wameanza kufahamiana jambo ambalo litawaandaa kuiendeleza Afrika Mashariki siku za usoni.
Mwenyekiti wa watanzania waishio Zimbabwe Apatae Fatacky amesema wazo hili lilianzishwa na Dada mmoja Raia wa Rwanda, waliobakia wamelifanyia kazi.
Post a Comment
Powered by Blogger.