Jamie Vardy Kuikosa Australia Dhidi Ya England Kisa Ndoa.

Mshambuliaji wa Leicester City Jamie Vardy atakosa mechi ya kirafiki ya Uingereza dhidi ya Australia siku ya Ijumaa kwa kuwa anafunga ndoa siku mbili kabla ya mechi hiyo.
Mchezaji huyo aliahirisha harusi yake mwaka uliopita na kuiahirisha tena mnamo mwezi Juni ili aweze kushiriki katika michuano ya Euro 2016.
Mkufunzi wa timu ya Uingereza Roy Hodgson alisema kuwa Vardy anahitaji muda ili kufunga ndoa yake.
Vardy ,aliyefunga bao la ushindi wa Uingereza dhidi ya Uturuki siku ya jumapili alisema:
Kocha amenipa hadi siku ya Jumatano ,lakini nitarudi mazoezini baadaye.
Post a Comment
Powered by Blogger.