Hivi Ndivyo Ilivyotokea Leo Wabunge Wanawake[UKAWA] Walivyotoka Bungeni.
Wabunge Wanawake kutoka Vyama vinavyounda Umoja wa Katiba
ya Wananchi (Ukawa) wamelazimika kutoka nje ya Ukumbi wa Bunge mjini
Dodoma baada ya Mbunge wa Ulanga Goodluck Mlinga kutoa kauli ya
udhalilishaji hapo jana.
Mbunge huyo alitoa kauli hiyo na kuwaambia wabunge wanawake
wa Chadema kwamba ili wapate Ubunge wa Viti Maalumu lazima waitwe
‘babe’.
Hayo yalijiri jana baada ya kuwepo kwa mvutano mkali hapo
jana baina ya wabunge wa chama tawala na upinzani kurushiana vijembe na
matusi ndani ya ukumbi wa bunge hali iliyopelekea Mbunge wa Jimbo la
Ukonga Mwita Mwikabwe Waitara kutolewa nje ya ukumbi huo baada ya
kutofautiana na Mbunge wa Ulanga Goodluck Mlinga.
Wabunge hao wanawake kutoka vyama mbalimbali vya upinzani
wamesisitiza adhma yao ya kujitoa katika Chama cha Wabunge Wanawake wa
Bunge la jamuhuri ya muungano kutokana na kutopewa ushirikiano na
wabunge wenzao wa chama tawala kwa madai kwamba wanaunga mkono
udhalilishaji wa wanawake bungeni kwani wakati hayo yakifanyika wao
walikuwa wakipiga makofi.