Huyu Ndo Rais Anayetuhumiwa Kwa Ufisadi Kupanda Kizimbani.

Rais wa zamani wa Brazil Lula Da Silva.
Mwanasheria mkuu wa Brazil,Rodrigo Janot,amemshutumu Rais wa zamani wa nchi hiyo Luiz Inacio Lula da Silva,kuhusika kwa kiasi kikubwa katika kashfa kubwa ya rushwa ya ufisadi inayoikumba kampuni ya mafuta ya Petrobras.
Rodrigo Janot.
Mwanasheria mkuu wa Brazil Rodrigo Janot.

Janot amesema rushwa hiyo inayokadiriwa kugharimu dola za kimarekani bilioni mbiliisingeweza kutokea kama sio kuhusika kwa Rais Lula.Janot ameitaka mahakama kuu kuidhinisha uchunguzi dhidi yake pamoja na wanasiasa wengine 29,wafanyakazi wa umma sambamba na wafanyabiashara.
Lula Da Silva.
Rais huyo wa zamani wa Brazil,Luiz Inacio Lula da Silva amekanusha madai hayo.
Post a Comment
Powered by Blogger.