Mwanamke Mfanyabiashara Anayeshtakiwa Kwa Ulanguzi Wa Pembe Jijini Dar es Salaam.

Huyu ndo mwanamke mfanyabiashara mkubwa raia wa China amfikishwa makahamani jijini Dar es Salaam kwa mashtaka ya kuendeleza mtandao wa kihalifu kwa ulanguzi wa pembe barani Asia.
Waendesha mashtaka wanasema Yang Feng Glan, anayejulikana kwa umaarufu pia kama Malkia wa pembe, aliendesha biashra haramu ya kuwaua ndovu katika mbuga za wanyama ili kupata pembe zao ambazo wanazisafirisha na kuziuza katika mataifa ya bara Asia.
Anashutumiwa kwa kuendeleza shughuli hiyo kwa takriban miaka 14 na amekana mashtaka hayo.

Maafisa wa serikali Tanzania wametaja kukamtwa kwa Yang Feng Glan mnamo Oktoba mwaka jana kama ufanisi mkubwa.
Taifa hilo la Afrika mashariki limepoteza thuluthi mbili za ndovu wake katika kipindi cha miaka kumi iliyopita.

Post a Comment
Powered by Blogger.