Huyu Hapa Mgombea Urais Wa Marekani Aliyejitoa Kwenye Kinyang'anyiro hicho Na Kumpa Donald Trump Urais.

Ted Cruz.
Seneta wa jimbo la Texas Ted Cruz amejiondoa katika kinyang'anyiro cha uteuzi kugombea nafasi ya urais wa Marekani kupitia chama cha Republican.
Mgombea Urais aliyejitoa Ted Cruz.

Alitoa tangazo lake punde tu baada ya kupoteza kura katika kampeni za mwisho Indiana.
Cruz amewaambia wafuasi wake kuwa alifanya kila analoweza katika kampeni zake,lakini hakukuwa na njia ya yeye kuweza kusonga mbele zaidi.
Mwandishi  aliyepo katika vituo vya kupigia kura Indiana amesema wafuasi wa Cruz wamestushwa na kukatishwa tamaa.
Donald Trump.
Tangazo hilo linatoa mwanya kwa Donald Trump kupata uteuzi wa chama chake cha Republican.
Post a Comment
Powered by Blogger.