Huku Akiwa Na Hofu Ya Kupinduliwa Na Marekani,Rais Maduro Mahakama Yasema Hajakiuka Katiba.


Rais wa Venezuela Maduro.

Mahakama kuu nchini Venezuela imesema agizo lililotolewa na Rais wa nchi hiyo Nicolas Maduro kutangaza hali ya hatari nchini Venezuela halikukiuka katiba.
Hatua hiyo inampa Maduro nguvu zaidi kushughulikia changamoto za kiuchumi, ikiwemo haki ya kudhibiti usambazaji wa Chakula na kuweka na kuchukua hatua za kulinda usalama.
Hatua hiyo ilipingwa vikali na upinzani siku ya Jumatano.
Lakini Mahakama kuu ambayo mara chache hutoa maamuzi dhidi ya Serikali ya kisoshalisti ya Venezuela imesema agizo hilo lilistahili kutokana na hali mbaya ya kiuchumi inayokumba taifa hilo.
Post a Comment
Powered by Blogger.