Hivi Ndivyo Liverpool Na Man City Hoi Zachakazwa Vibaya Huku Ayew Na Mane Hawashikiki.

Mane na Andre.


Mshambulizi wa Black Stars ya Ghana Andre Ayew alifunga mabao mawili na kuisadia timu yake ya Swansea kujihakikishia nafasi katika ligi kuu ya Uingereza msimu ujao.

Ayew alifunga mabao hayo Swansea City ilipojifurukuta na kuiadhibu Liverpool 3-1.
Andre Ayew.

Ayew alifungua kibano hicho kwa mkwaju wa kichwa kabla ya Jack Cork kufuma kimiani mkwaju ulioipa swansea uongozi wa mabao mawili kwa nunge kufikia muda wa mapumziko.
Hata hivyo vijana wa Jurgen Klopp walirejea uwanjani kwa kishindo.
Christian Benteke alirejeshea Liverpool matumaini kwa kufunga bao mapema katika kipindi cha pili.
Lakini Ayew akawazimia nuru kabisa katik mechi hii alipofunga bao lake la tatu na la ushindi dakika mbili tu baadaye kunako dakika ya 67.
Masaibu ya Liverpool yaliongezeka Brad Smith alipooneshwa kadi yake ya pili ya njano na hivyo kulazimika kuiaga mechi hiyo.
Kufuatia kichapo hicho Liverpool sasa haina budi kuingia ukanda iliangalau waweze kushinda kombe la Europa iwapo bado wanamatumaini ya kushiriki katika kombe la mabingwa barani ulaya mwakani.
Kwa upande wao Swansea, ambao wanaorodhewshwa katika nafasi ya 13 wamejizolea alama 11 zaidi ya Sunderland ambayo iko katika hatari kubwa ya kushushwa daraja msimu ujao.
Wakicheza ugenini timu ya Man City walipokea kichapo cha mbwa mwitu wakitandikwa bao 4-2 na wenyeji Southmpton huku mabao matatu yakifungwa na mshambuliaji wa Senegal Said Mane na Long.
Said Mane.
 Vinara wa ligi hiyo Leicester City wakiwa ugenini walilazimishwa sare na wenyeji Man United ya 1-1 na kushindwa kutangazwa mabingwa kwani kwa sasa wanahitaji pointi mbili iliwaweze kufikisha pointi 79 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote endapo leo kama Tottenham atapoteza au kutoka sare na Chelsea watatangazwa mabingwa wapya msimu huu.
Post a Comment
Powered by Blogger.