Hiki Hapa Kilichomuua Mkurugenzi Wa Jiji La Dar es Salaam Wilson Kabwe Familia Yaeleza.
Ikiwa watu wengi wamebaki na maswali kichwani juu ya nini hasa kiliutoa uhai wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Wilson Kabwe, mtoto wake amezungumza juu ya tatizo la baba yake na kilichoutoa uhai wake.
Mtoto wa marehemu, Geofrey Kabwe alisema kuwa baba yake alianza kuugua maradhi ya tumbo Julai mwaka jana na aliendelea kupokea matibabu hapa nchini. Lakini Desemba alizidiwa na familia iliamua kumpeleka India kwa matibabu zaidi.
Akiwa nchni India, Madaktari waliokuwa kimpatia matibabu waliambiwa kuwa tatizo liko kwenye Ini na kilichosababisha Ini hilo kupata matatizo zaidi ni dawa alizokuwa akizitumia. Alipatiwa matibabu na kupona kabisa na Januari alirejea nchini akiwa na afya njema na alianza kwenda kazini Februari huku akihudhuria kliniki katika Hospitali ya Apollo nchini India.
Aliporejea kazini baada ya muda mchache hali yake ilianza kubadilika na tukaingiwa na hofu. “Wiki mbili zilizopita nilipigiwa simu nikiwa Arusha nikaelezwa kwamba hali yake kiafya siyo nzuri, tulimwona daktari wake na akabainika kuwa na Pneumonia (homa ya mapafu), tulimhamishia TMJ kwa ajili ya kipimo cha CTScan, matokeo yalionyesha kuwa ini lilikuwa limeharibika na tayari mwili ulikuwa umeanza kuvimba lakini pia alikua akisumbuliwa na tatizo la Saratani ya Tezi Dume. Ilipofika saa mbili usiku hali ilibadilika akawa anakoroma na saa tatu usiku akafariki dunia.”- Geofrey Kabwe
Aidha msemaji wa familia, Dk Machuve alieleza taratibu za mazishi kuwa “Atasafirishwa kwenda kuzikwa nyumbani kwake Jumanne jioni baada ya kuagwa nyumbani kwake Masaki. Mazishi yanatarajiwa kufanya kijijini Mamba Mpinji, Same Kilimanjaro Jumatano.”
Mkurugenzi huyo Wilson Kabwe alisimamishwa kazi April 19, 2016 na Rais Dkt Magufuli alipokua kwenye uzinduzi wa Daraja la Nyerere kwa tuhuma za kusaini mkataba kwa kutumia sheria ndogo ya mwaka 2004 kutoza magari yanayotoka kwenye Kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo (UBT) Sh4,000 huku akidaiwa kusaini mkataba mwingine wa Sh8,000 chini ya sheria ndogo ya mwaka 2009 na masuala mengine ya ufisadi.
Post a Comment
Powered by Blogger.