Hiki Hapa Kikosi Kipya Cha Taifa Stars Mkwasa Akitaja Huku Akimtema Kelvin Yondani Na Canavaro Ndani.

Kocha wa Taifa Stars Charles Bonifance Mkwasa
Kocha Mkuu wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa ametangaza kikosi kitakachomenyana na Kenya Mei 29 uwanjani Kasarani, Nairobi.
Mchezo huo ni sehemu ya maandalizi kwa timu zote mbili kujiandaa kwa michezo ya kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Bingwa Afrika mapema mwezi Juni, 2016.
TFF kwa kushirikiana na FKF zimekubaliana kuwepo kwa mchezo huo wa kirafiki, utakotumika kama sehemu za maandalizi kwa timu zote kujiandaa na michezo ya kuwania kufuzu kwa AFCON 2017 mwezi Juni.
Taifa Stars inatarajiwa kuingia kambini Mei 22, mara baada ya kumalizika kwa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kujiandaa na mchezo huo wa kirafiki kabla ya kuwakabili Misri katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Juni 4, mwaka huu.
Kikosi  Kamili kama ifuatavyo:

Makipa: Deo Munishi ‘Dida’ (Yanga SC), Aishi Manula (Azam FC), Beno Kakolanya (Prisons FC).

Mabeki: Nadir Haroub ‘Cannavaro’ (Yanga SC), Aggrey Morris (Azam FC), Erasto Nyoni (Azam FC), David Mwantika (Azam FC), Juma Abdul (Yanga SC), Mwinyi Hajji Mngwali (Yanga SC) na Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ (Simba SC).

Viungo: Himid Mao, Mohammed Ibrahim (Mtibwa Sugar), Shizza Kichuya (Mtibwa Sugar), Jonas Mkude (Simba SC), Ismail Issa Juma (JKT Ruvu), Mwinyi Kazimoto (Simba SC), Farid Mussa (Azam FC), Juma Mahadhi na Hassan Kabunda (Mwadui FC).


Washambuliaji: Thomas Ulimwengu (TP Mazembe – DRC), Mbwana Samatta (KRC Genk – Ubelgiji), Elias Maguri (Stand United), Ibrahim Hajib (Simba SC), John Bocco (Azam FC), Deus Kaseke (Yanga SC) na Jeremiah Juma (Prisons).

Post a Comment
Powered by Blogger.