Hii Hapa Kauli Ya Rais Magufuli Kuhusu Vifo Vya Watu Saba Waliokatwa Mapanga.

Rais wa Tanzania John Magufuli.
Rais Dk. John Magufuli amesikitishwa na mauaji ya kinyama ya watu saba wa familia moja waliokatwa mapanga katika Kijiji cha Sima wilayani Sengerema mkoani Mwanza.

 Rais Magufuli ameviagiza vyombo vya dola kuwasaka kwa nguvu zote, watu waliohusika na mauaji hayo na kuhakikisha wanatiwa mbaroni ndani ya kipindi kifupi.
Makamu wa Rais Wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

Akitoa salamu za pole nyumbani kwa wafiwa jana, Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan,
alisema Rais Magufuli ameguswa na tukio hilo
na kusema umefika wakati wa wananchi kumwabudu Mungu ili maovu kama hayo yasitokee.

“Wakati nakuja huku, Rais Magufuli amenituma  nimfikishie salamu zake za rambirambi kwa ndugu, jamaa na marafiki mliofiwa.

“Ameagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha vinawasaka na kuwatia mbaroni watu waliohusika na tukio la kinyama ili wafikishwe kwenye vyombo vya sheria,” alisema.

Alisema Rais Magufuli ametaka wahusika wote wakamatwe ndani ya kipindi kifupi, kwa sababu
mauaji ya aina hiyo hayakubaliki hata kidogo.

Samia alisema Rais Magufuli amewataka wananchi kumcha Mungu kwa kuwa wakishika imani na kumwabudu maovu yatapungua.

Alisema jamii ya wacha Mungu haina maovu mengi kama hayo.
Kuwasili kwa Samia katika msiba huo, kuliamsha vilio vingi kutoka kwa wananchi waliokuwapo.

Samia alitembelea sehemu ambayo ujenzi wa makaburi matano ulikuwa unaendelea kwa
gharama za Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema.
Post a Comment
Powered by Blogger.