Haya Ndo Maamuzi Ya Mahakama Kuhusu Rufaa Ya Harry Kitilya,Shose Sinare Na Sioi Solomoni.


Rufaa ya kupinga kufutwa kwa shitaka la nane katika kesi inayowakabili Harry Kitilya, Shose Sinare, Sioi Solomoni imekataliwa na Mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Dar es Salaam.


Shitaka la nane katika kesi hiyo lilikuwa ni la utakatishaji fedha  lililofutwa na Hakimu Emillius Mchauru  katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliyopelekea upande wa mashitaka kutoridhika na maamuzi hayo.

Akitoa maamuzi hayo  Hakimu Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam Moses Mzuna, amesema kuwa rufaa hiyo haina mashiko kisheria.
Hata hivyo Hakimu Mzuna amefuta rufaa hiyo na kwamba kesi hiyo itaendelea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu huku akimshauri Timon Vitalis kuendelea na kesi hiyo na endapo kesi hiyo itafika mwisho bila kuridhika na maamuzi wataruhusiwa kukata rufaa.
Post a Comment
Powered by Blogger.