Haya Ndo Maamuzi Ya CCM Kuhusu Charles Kitwanga.

Chama cha Mapinduzi [CCM] kimetoa tamko rasmi kuhusu adhabu iliyotolewa na Rais John Pombe Magufuli kumuondoa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya ndani Mh.Charles Kitwanga katika katika nafasi hiyo baada ya kuingia bungeni akiwa amelewa na kushindwa kujibu maswali kwa ufasaha.
Christopher Ole Sendeka.
Msemaji wa chama hicho mh.Christopher Ole Sendeka alisema kuwa chama hicho kinatoa pongezi kwa Rais Magufuli kwa uamuzi huo aliouchukua lakini chama hakitamuadhibu Kitwanga kwa kuwa adhabu huwa haitolewi mara mbili.
Ole Sendeka alibainisha kuwa uamuzi huo nifundisho kwa wanachama wote ambao ni watumishi wa umma kutokiuka miiko ya uongozi.
''Hatutasita kuchukua hatua endapo tutabaini kuna mwanachama anayekiuka maadili ya uongozi wa umma''alisema Ole Sendeka.
Mh.Kitwanga aliondolewa katika nafasi hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita wakati ambapo bado alikuwa akituhumiwa na kujihusisha na sakata la mkataba tata kati ya jeshi la polisi na kampuni ya Lugumi Enterprise.
Post a Comment
Powered by Blogger.