DK.Kiiza Besigye Apelekwa Gereza La Kampala Baada Ya Kujiapisha Kuwa Rais Wa Uganda.

Kiongozi wa upinzani nchini Uganda Kizza Besigye anahamishwa kutoka gereza la Moroto Kaskazini Mashariki mwa nchi kwenda gereza la Luzira lililo mji mkuu Kampala ambalo ndilo gereza kubwa zaidi nchini humo.
Bw.Besigye akijiapisha kuwa Rais wa Uganda.
Msemaji wa Idara ya magereza nchini Uganda Frank Baines amethitisha kuwa bwana Besigye kwa sasa yuko njiani kwenda Kampala.
Siku ya Ijumaa alishtakiwa kwa uhaini na kupelekwa rumande huko Moroto baada ya kukamatwa mjini Kampala.
Video moja imekuwa ikisambaa kwenye mitandao ya kijamii ikimuonyesha Besigye akijiapisha kuwa rais.
Post a Comment
Powered by Blogger.