DK.KIIZA BESIGYE AKAMATWA KWA KUJIAPISHA KUWA RAIS UGANDA.

Taharuki imetanda nchini Uganda baada ya kiongozi wa upinzani Dr Kizza Besigye, ''kujiapishwa kama rais'' siku moja tu kabla ya kuapishwa rasmi kwa rais Yoweri Museveni .
Haijulikani ni vipi Dr Kiiza Besigye alikwepa kizuizi cha polisi na kuibukia mjini Kampala ambapo alikutana na wandani wa chama chake na ''kula kiapo cha urais wa taifa hilo''.
Katika video inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii Dr Besigye anaonekana ''akila kiapo'' mbele ya mtu aliyevalia mavazi sawa na ya ''jaji wa mahakama ya juu''.
Video hiyo imesambazwa mno kwenye mitandao ya kijamii na kusababisha mamlaka inayosimamia mawasiliano nchini Uganda kuamrisha kampuni zinazotoa huduma za simu nchini humo kufunga huduma za mitandao ya kijamii.
Besigye anahitimisha 'kuapishwa kwake'' kwa kuonya kuwa ''endapo kutafanyika sherehe nyengine hapo kesho, basi itakuwa ni kinyume cha sheria kwani kulingana naye Museveni hakushinda uchaguzi wowote''.
Mgombea huyo wa kiti cha urais kwa tiketi ya chama cha upinzani cha Forum for democratic change FDC- alikamatwa na polisi kwa'' kukaidi amri halali''.
Matukio hayo yanawadia wakati ambao viongozi wa kanda ya Afrika Mashariki na wageni mashuhuri wameanza kuwasili mjini Kampala ilikuhudhuria kuapishwa kwa rais Museveni hapo kesho.
Tangu matokeo ya uchaguzi kutangazwa mwezi Februari, Dr Kiiza Besigye amekuwa chini ya ulinzi mkali nyumbani kwake baada ya kupinga matokeo yaliyompa rais Museveni ushindi.
Post a Comment
Powered by Blogger.