Maamuzi Ya BASATA Kuhusu Chura Ya Snura.
Mwanamziki Snura.
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na michezo kwa kushirikiana na vyombo vingine vinavyoshughulika na sanaa ikiwemo BASATA wamekubaliana kuufungia wimbo na video ya Chura kupigwa kwenye vyombo vya Habari, maeneo ya hadhara na mahala popote kwenye mkusanyiko wa watu.


Serikali kupitia muwakilishi wake imedai kuwa, wimbo huo unadhalilisha na kukiuka haki za binadamu.

Wizara pia imebaini kuwa Msanii Snura, hana nyaraka maalum za kujihusisha kwenye masuala ya muziki, hivyo imemfungia kujihusisha na matamasha ya aina yoyote mpaka pale atakapotimiza taratibu.
Post a Comment
Powered by Blogger.