Baada Ya Yanga Kupangwa Na TP Mazembe,Hans Van Der Pluijm Na Niyonzima Wametoa Maneno Haya.

Yanga.
Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya kombe la shirikisho klabu ya soka ya Yanga imepangwa kundi moja na timu ya Tp Mazembe.
Hatua hii ya nane bora imegawanywa katika makundi mawili yenye timu nne kila kundi ambapo kundi A kuna timu za Yanga ya Tanzania ,Tp Mazembe ya Jamuhuri ya kidemocrasia ya Congo,Mo Bejaia ya Algeria na Medeama ya Ghana.
Huku Kundi B likiwa na timu mbili za kutoka nchini Morocco ambazo ni Kawkab na Fus Rabat na pia kuna Etoile du Sahel ya Tunisia na Ahly Tripoli kutoka nchini Libya.
Hans Van Der Pluijm na Msaidizi Wake Juma Mwambusi.
Kocha mkuu wa klabu ya Yanga Mdachi Hans Van Der Pluijm,mara ya kuona wapinzani wake kwenye kundi A,amesema kuwa amefurahi kukutana na mabingwa wa Afrika TP Mazembe kwani anawajua vilivyo na alishawahi kukutana nao mara nne akiwa na Berakum Chelsea ya Ghana na alishinda mechi tatu na kufungwa moja hivyo hakuna cha kuogopa Yanga ni timu bora ndo maana imefika hapo.
Kila mtu anaamini kuwa katika timu nane zilizoingia kibonde ni Yanga kwa vile inatoka Tanzania ila tunaamini tutaushangaza ulimwengu wa soka kwa kufuzu hatua ya nusu fainali kinachotakiwa na kuandaa kikosi chetu kwa mechi yote iliyo mbele yetu na tutajua leo baada ya fainali yetu na Azam katika uwanja wa Taifa.
Haruna Niyonzima.
Kwa upande wa kiungo bora kabisa Afrika Mashariki na Kati Haruna Niyonzima,amesema kuwa hapo walipofika hakuna timu ya kuiongopa kweli kwenye kundi letu ni gumu na tunaziheshimu timu zote wapo Mazembe ambao ni mabingwa wa Afrika kwa sasa Yanga ni timu kubwa inawachezaji wenye njaa na mafanikio tunamuomba mungu atusaidie tutafika mbali kikubwa ni maandalizi nje ya uwanja na ndani ya Uwanja.
 
Mechi ya kwanza Yanga ataanzia ugenini kucheza na waarabu nchini Algeria timu ya Mo Bejaia  kati ya Juni 17 na 19, na mechi ya pili atakuwa nyumbani kucheza na TP Mazembe  kati ya Juni 28 na 29,mechi za Makundi zitamalizika tarehe 23 na 24 Agosti na washindi wawili wa kila kundi kutinga nusu fainali.
Post a Comment
Powered by Blogger.