Baada Ya Kutekwa Miaka 2 Iliyopita Na Boko Haramu Wanafunzi Wa Chibok Mmoja Apatikana Akiwa Na Mimba Nigeria.

Wanaharakati nchini Nigeria wanasema kuwa mmoja wa wasichana wa shule wa Chibok, waliotekwa nyara na kundi la Boko Haram amepatikana, akiwa ndiye mtu wa kwanza kukolewa kwa zaidi ya miaka miwili.
Zaidi ya wasichana 200 walitekwa nyara na wanamgambo wa Boko Haram kutoka mji ulio Kaskazini Mashariki mwa Nigeria zaidi ya miaka miwili iliyopita.
Mwanaharakati Hauwa Abdu aliiambia BBC kuwa, msichana huyo alipatikana siku ya Jumanne jioni na kundi moja la kuweka ulinzi baada ya makabiliano na watu wanaokisiwa kuwa wapiganaji wa Boko Haram.
Kiongozi mmoja wa kijamii alisema kuwa msichana huyo alikuwa na mtoto na wote wamekabidhiwa jeshi la Nigeria katika mji wa Damboa.
Post a Comment
Powered by Blogger.