Baada Ya Kupata Ushindi Dhidi Ya Simba,Kocha Wa Mwadui Jamhuri Kihwelo Julio Ametoa Maneno Mazito.

Kocha wa Mwadui Jamhuri Kihwelo Julio.
Kocha mkuu wa timu ya Mwadui Jamhuri Kihwelo Julio,baada ya kupata ushindi wa 1-0 dhidi ya Simba katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jana katika mwendelezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara.
Jamhuri Julio.
Julio amesema kuwa Simba wanajitakia wenyewe kutokana na kupenda kuleta makocha ambao hawana uwezo pamoja na benchi nzima la ufundi huku akiendelea kulalamika kutokana na timu hiyo yake ya zamani kuwa wana laana ya kuwatimua yeye pamoja Abdalah Kibandeni bila kuwapa fedha zao.
Mwadui.
Alendelea kusema uongozi huu uliopo kwa sasa hawajui kuendesha soka ndo maana timu inaendelea kufanya vibaya kwani yeye na Kibandeni walijiwekea malengo ya kuwa msimu ambao walitimuliwa kama ngunia la mkaaa walitaka timu ishike nafasi ya tatu au ya pili ili msimu unaokuja chakushangaza walifukuzwa bila kupewa malipo hivyo dhulumu hiyo itaendelea kuwatesa Simba.
Simba.
Kikosi cha Smba kilicheza vizuri ila washambuliaji wake hawakuwa makini kutokana na nafasi walizozipata walishindwa kuzitumia hatimaye wakakubali kufungwa bao 1-0 lililofungwa na Jamal Mnyate huku wakishushwa na Azam hadi nafasi ya tatu na watani zao Yanga wakitawazwa kuwa mabingwa wapya kwa msimu 2016/17 kwa mara ya pili mfululizo.
Post a Comment
Powered by Blogger.