Aston Villa Yauzwa Huku Tajiri Akisema Maneno Haya.

Aston Villa.


Mfanyabiashara wa China aliyeinunua klabu ya Aston Villa ya nchini Uingereza amesema kuwa ana mipango kabambe juu ya klabu hiyo.
Tony Xia.
Tony Xia, anayemiliki kampuni ya Recon inayoshughulika na masuala ya Ugavi, anataka klabu hiyo irejee ligi kuu na kisha kumaliza ndani ya sita bora.
Imeripotiwa kuwa ametumia zaidi paundi milioni 60 kununua timu hiyo ambayo ilishushwa daraja baada ya kuwa na msimu mbovu. Wakati huo huo mmiliki wa klabu ya Leicester City Vichai Srivaddhanaprabha ambao wameishangaza dunia kwa kushida taji la ligi kuu soka England wamewasili na kupokelewa kwa heshima mjini Bangkok wakitarajiwa kufanya ziara kwa kutumia basi la wazi katika mji huo mkuu wa Thailand.
Post a Comment
Powered by Blogger.