Angalia Ratiba Ya Kuu Ya Vodacom Ni Vita Ya Kushuka Daraja Na Kesho Ni Vita Ya Simba Na Mwadui Ya Julio Taifa.

Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara kuendelea tena leo katika viwanja vitatu nyasi zake kuwaka moto kwa ajili ya kuelekea kumaliza msimu wa ligi kuu.
Katika uwanja wa Mabati JKT Ruvu watacheza na Ndanda,huko katika uwanja wa Kambarage Shinyanga wapiga debe timu ya Stand United watacheza na Coast Union ambao tayari wameshuka daraja na katika uwanja wa Mkwakwani Tanga pointi tatau muhimu kwa Mgambo JKT watacheza na Mtibwa Sugar.
Simba.
Ligi hiyo itaendelea siku ya Jumapili kwa michezo miwili kuchezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kutakuwa na vita ya kufa kupona wekundu wamsimbazi Simba watacheza na Mwadui ya kocha wa maneno mengi Jamhuri Kihwelu Julio na Katika uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga kesho itakuwa hatima ya Kagera Sugar kubaki ligi kuu msimu ujao ama kushuka daraja watakapocheza na matajiri wa jiji la Dar es Salaam timu ya Azam.

Post a Comment
Powered by Blogger.