Angalia Jinsi Mwanamuziki Huyu Alivyopigwa Marufuku Na Twitter.

Mwanamuziki Azealia Banks.

Mwanamuziki wa mtindo wa Rap Azealia Banks amepigwa marufuku na mtandao wa Twitter.
Nyota huyo wa 212 amezuiliwa kuingia katika mtandao huo kufuatia hatua yake ya kutumia mtandao huo kumtusi msanii Zayn Malik.
Msanii Zayn Malik.

Ameshtumiwa kwa ubaguzi baada ya kufananisha mizizi ya mwanamuziki huyo mbali na kutumia matusi.
Zayn Malik.

Kufuatia matamshi yake dhidi ya Zayn,ameondolewa katika tamasha la Born and Bred mjini London.
Gazeti la Metro limeripoti kwamba wizara ya maswala ya ndani nchini humo ilikuwa na mpango wa kumpiga marufuku mwanamuziki huyo kutoingia Uingereza.
Azealia Banks.
Ukurasa wake wa Twitter kwa sasa unaonyesha kwamba amepigwa marufuku na kwamba akaunti yake imeondolewa katika mtandao huo.
Post a Comment
Powered by Blogger.