Angalia Hapa Mchuano Ni Mkali Bernie Sanders Amchakaza Hillary Clinton Mchujo.

Bernie Sanders.
Seneta wa Vermont Bernie Sanders amemshinda Hillary Clinton kwenye uchaguzi wa mchujo wa kuteua mgombea urais wa chama cha Democratic katika jimbo la Indiana.
Sanders amemshinda Clinton kwa kura chache.
Matokeo hayo hayaathiri sana uongozi wa jumla wa Bi Clinton na bado anapigiwa upatu kushinda uteuzi wa chama hicho.
Clinton na Sanders.
Bw.Sanders amesema bado ataendelea na kampeni "Watu wa Clinton wanadhani kampeni yetu imefikia kikomo. Wamekosea,” amesema Bw Sanders.
Baada ya kujiondoa kwa seneta wa Texas Ted Cruz kutoka kwa kinyang’anyiro cha kutafuta mgombea urais katika chama cha Republican, kuna uwezekano mkubwa kwamba huenda mwishowe Bw Trump akawa anakabiliana na Bi Clinton.
Uchaguzi mkuu utafanyika Novemba kumchagua mrithi wa Rais Barack Obama wa chama cha Democratic anayeondoka White House baada ya kuongoza kwa mihula miwili.
Post a Comment
Powered by Blogger.