Yanga Haikamatiki Yaifumua Vibaya Mwadui Ya Julio Na Kuikaba Koo Simba Matokeo Yapo Hapa.

MTN ya Yanga.
Mabingwa watetezi wa ligi ya Vodacom Tanzania bara imewakaribisha vijana wa Mwadui mchezo uliochezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam huku Yanga wakiibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Mwadu.
Simon Msuva akishangilia bao lake.
Mchezo ulianza kwa mashambulizi ya kushitukiza mnamo dakika ya tatu ya mchezo Simon Msuva aliiandikia bao timu yake kwa pasi nzuri kutoka kwa mshambuliaji hatari wa Yanga Donald Ngoma,vijana wa mwadui walisawazisha kupitia kwa kelvin Hisabati kutokana na usembe wa kiungo wa Yanga Thabani Kamusoko kupiga pasi ovyo iliyonaswa na adui.
Mwadui.

Baada ya kupata bao timu ya mwadui ilicharuka na kuisumbua ngome ya Yanga ambayo muda wote ilikuwa iliyumba kutokana Cavaro kutokuwa na maelewano na beki mwenzake Pato Ngonyani hadi mapumziko zilikwenda zikiwa zimefungana bao 1-1.
Yanga.
Kipindi cha pili kilianza kwa Yanga kwa kufanya mabadiliko kwa kuwatoa Pato Ngonyani na Abubakari Yussuph na nafasi zao zilichukuliwa na Mwashuya na Vicent Bossou mnamo dakika ya 26 Juma Mobi alitolewa kwa kadi nyekundu baada ya kumchezea madhambi Ngoma.
Haruna Niyonzima.
Mnamo dakika ya 87 kiungo haruna Niyonzima aliandikia bao la pili timu yake akipokea pasi kutoka kwa Ngoma hadi dakika 90 zinakwisha Yanga wakiibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Kwa ,atokeo hayo Yanga wamefikisha jumla ya pointi 56 na kuwakaribia vinara wa ligi timu ya Simba yenye pointi 57 ikiwa imecheza mechi 24 huku Yanga wakiwa wamecheza mechi 23 na siku ya jumapili watacheza na timu ya Mtibwa Sugar.
Powered by Blogger.