Wolfsburg Yaishangaza Dunia Yaichakaza Vibaya Real Madrid Na PSG Yabanwa Na Man City.

Kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane.

Ligi ya mabingwa barani Ulaya imeendelea kwa michezo miwili ya robo fainali kuchezwa katika nchi mbalimbali vita kubwa ilikuwa nchini Ufaransa na Ujerumani.
Wolfsburg wakiwa katika uwanja  wao wa nyumbani katika dimba la Volkswagen Arena,wamewachakaza vibaya mabingwa wa kihistori  2-0 dhidi ya Real Madrid.
Ricardo Rodriguez.
Wolfsburg walianza kupata dakika ya 18 Ricardo Rodriguez ndiye alianza kuipatia timu yake bao la kwanza kwa mkwaju wa penati baada ya Andre Schurrle kufanyiwa madhambi na Casemiro.
Andre Schurrle.
Katika dakika ya 25 Max Arnold akaongeza bao la pili na kuwazamisha kabisa vijana wa Zidane.
Max Arnold.
Wakiwa katika ugenini  Man City wakicheza  huko nchini Ufaransa walikwenda sare ya kufunga kwa mabao 2-2, mabao ya Psg yalifungwa na mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic na Adrien Rabiot hata hivyo Zlatan Ibrahimovic alikosa mkwaju wa penati iliokolewa na Joe Hart.
Zlatan Ibrahimovic.

Adrien Rabiot.
Huku mabao ya Man City yakifungwa na viungo Kevin De Bruyne na Fernandinho,na kujiweka katika nafasi nzuri ya kusonga mbele ya michuano hiyo.
Kevin De Bruyne.
Fernandinho.

  Published By: Alex Sonna.

 Unaweza Kuzipata Story Zote Za Ndani Na Nje Ya Bongo Kwa Kujiunga Na SeetheAfricanLink Kwenye: Facebook|Twitter|Instagram|YouTube|Audiomack

Powered by Blogger.