Ujumbe Mzito Wanaswa Kaburini Kwa Kanumba


IMG_3360Ujumbe uliokutwa kaburini kwa Kanumba.
Stori:  Mayasa Mariwata na Gladness mallya, Ijumaa
Wakati mama yake, Flora Mtegoa (pichani), baadhi ya wasanii na mashabiki wake wakikumbuka miaka minne ya kifo cha aliyekuwa staa mkubwa wa filamu za Kibongo, Steven Charles Kanumba ‘The Great’, kumezuka sintofahamu ya kukutwa ujumbe mzito wa kimapenzi kaburini kwa msanii huyo ambao unadaiwa kuwekwa na mrembo aliyefika mahali hapo mapema wiki hii.

TUJIUNGE MAKABURI YA KINONDONI
Kwa mujibu wa mtu aliyedai ni mmoja wa walinzi wa Makaburi ya Kinondoni, Dar, alikolazwa Kanumba kwenye nyumba yake ya milele, ishu hiyo ilijiri Jumanne wiki hii, majira ya jioni ambapo mwanadada huyo alionekana akishuka kwenye gari (halikutajwa ni aina gani) na kuelekea kaburini hapo.

IMG_3335Mrembo aliyekutwa kaburini.
Alisema kuwa, huku akiwa amejitanda mtandio na maua mkononi, baada ya kufika kaburini hapo alionekana akiangua kilio na kuangusha maombi mazito kabla ya kuacha ujumbe na kuondoka zake.
BOFYA HAPA KUKISIKIA CHANZO
“Haloo…naongea na Ijumaa? Njooni wenyewe mjionee kuna mtu yuko hapa kwenye Kaburi la Kanumba, lakini kajifunika sana hadi usoni.

“Mimi nimeshindwa kumbaini ni nani japokuwa kwa mtazamo wa haraka anaweza kuwa huyu Lulu (mwigizaji Elizabeth Michael) na hata wengi waliomuona wanadai huenda akawa ni yeye ila mimi sina uhakika kwa sababu sipo karibu na wasanii.
“Nimemuona akilia sana kisha akaweka kikaratasi na maua na kuondoka zake.
“Nimejaribu kumpiga picha kwa simu yangu labda ninyi mkija mnaweza kumtambua kwa hizi picha na kujionea wenyewe kilichoandikwa kwenye karatasi aliyoiacha maana kinashangaza,” alisema jamaa huyo na kuongeza:
“Unajua siyo yeye tu, mara kwa mara kuna watu huwa wanakuja sana kaburini kwa Kanumba. Ni utaratibu wa kawaida sana kwa watu kuja kuwatembelea wapendwa wao hapa lakini huyu alionekana kuwa tofauti kwa kujifichaficha na huo ujumbe aliouacha.

elizabethmichaelofficial_78Mwigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’.
IJUMAA MZIGONI
Baada ya kunyetishiwa tukio hilo, Ijumaa liliingia mzigoni ambapo bila kupoteza muda lilifika eneo la tukio ndani ya muda mfupi kwa kutumia bodaboda ziendazo kasi ili kukwepa foleni za jijini Dar ambapo lilipishana na mwanadada huyo kwenye gari akiondoka bila kumshtukia.
Hata hivyo, mapaparazi wetu waliambulia kuusoma ujumbe walioukuta kaburini hapo ambapo sehemu fupi ilisomeka:

UJUMBE WENYEWE
“Ni mwaka wa nne huu tangu umenitoka, upendo wako kwangu ulinifanya niwe wa kipekee hapa duniani, leo hii ungekuwa hai huenda tungekuwa mke na mume na tungekuwa na watoto lakini Mungu hakupenda hilo litokee. Nakukumbuka na nitakupenda daima. Pumzika kwa amani…”.

Baada ya kuuona ujumbe huo, Ijumaa lilimrudia mtoa habari huyo aliyeomba hifadhi ya jina ambaye alionesha picha hizo kwenye simu yake kabla ya kumrushia mmoja wa mapaparazi wetu.
NI LULU?
Hata hivyo, katika kuzitathmini picha hizo, mapaparazi wetu nao walishindwa kung’amua kama ni Lulu au ni staa gani mwingine aliyewahi kuwa mwandani wa Kanumba.

28Mama wa marehemu Kanumba, Flora Mtegoa.
Wengine waliowahi kudaiwa kutoka na Kanumba ambao huenda mmoja wao anahusika na ujumbe huo ni Wema Sepetu, Sylivia Shally, Aunt Ezekiel, Shamsa Ford, Agnes Gerald ‘Masogange’ na mastaa wengine wakiwemo pia wanawake wawili walioibuka na kudai wamezaa na staa huyo waliofahamika kwa majina ya Salma na Pascalia.
Ili kuweka sawa mzani wa habari hiyo, gazeti hili liliona ni vyema kumvutia waya Lulu ambaye anahisiwa kuwa ndiye aliyeweka ujumbe huo. Hata hivyo, simu yake ilionesha ipo ‘bize’ muda wote. Alipotumiwa ujumbe mfupi wa maneno (SMS) hakujibu.
HUYU HAPA MAMA KANUMBA
Kwa upande wake, mama Kanumba alipoulizwa kuhusu ishu hiyo alifunguka kuwa, licha ya kuwa imepita miaka minne tangu kifo cha mwanaye lakini hawezi kumsahau hadi naye atakapokutwa na umauti.
Kuhusu mwanamke aliyeonekana kaburini kwa Kanumba ikidhaniwa kuwa ni Lulu alikuwa na haya ya kusema:
“Kama wanasema ni Lulu inawezekana, nadhani labda aliamua kwenda siku hiyo kwa kuwa hakutaka kushiriki na mimi kwa sababu nashindwa kumhisi mtu mwingine kwa kuwa Kanumba alikuwa msiri sana. Mwanamke aliyewahi kunitambulisha ni staa mmoja tu na si Lulu.”

Steven-KanumbaMarehemu Steven Kanumba enzi za uhai wake.
KUMBUKUMBU MUHIMU
Kanumba alifariki dunia Aprili 7, 2012 kwa kuanguka katika mazingira yaliyodaiwa kutokana na ugomvi kati yake na Lulu. Tukio hilo lilitokea nyumbani kwa Kanumba, Sinza ya Vatcan, Dar.
Baada ya kifo hicho, Lulu alikamatwa na kuwekwa Mahabusu ya Segerea jijini Dar na baadaye kuachiwa kwa dhamana ambapo kesi hiyo bado inasubiriwa kuanza kuunguruma.

Baada ya kutoka mahabusu, Lulu na mama yake, Lucresia Karugila walimfuata mama Kanumba na kuomba msamaha ambapo mama huyo aliupokea na kusema anamwona Lulu kama mtoto wake na yote ya nyuma yamepita.
Kuanzia hapo, Lulu na mama Kanumba wakawa na ukaribu wa kindugu huku kila mwaka wakifanya kumbukumbu ya Kanumba pamoja kabla ya mwaka jana kutibuana.
CHANZO: GLOBAL PUBLISHERS
Powered by Blogger.