Uhondo Wikendi Hii Ratiba Ya Ligi Ya Vodacom Tanzania Bara Simba Na Yanga Vitani.

Nembo ya Vodacom.
Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara kuendelea tena wikendi hii kwa michezo mitatu nyasi kuwaka moto katika miji mbalimbali nchini.
Yanga.
Katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam kutakuwa na kazi kubwa mabingwa watetezi wa ligi hiyo timu ya Yanga watakuwa wenyeji wa Mtibwa Sugar kutoka Morogoro huu ukiwa ni mchezo wa kiporo na kama Yanga watashinda watafikisha jumla ya pointi 59 kwa michezo 24 huku wakiingia kwa kumbukumbu ya ushindi kutoka kwa Mwadui 2-1.


Mtibwa Sugar.
Klabu ya Mtibwa Sugar wataingia kwa kumbukumbu ya kufungwa bao 1-0 dhidi ya matajiri wa jiji Azam FC na tayari msemaji wa Mtibwa Tobias Kifaru amejinasibu kuwa watawalaza mapema Yanga mbele ya mashabiki wake watakaofurika lazima watoke na maumivu.
Ndanda FC.
Mjini Mtwara kutakuwa na shughuli katika uwanja wa Sijaona wenyeji Ndanda kuchele watacheza na wauza Sukari timu ya Kagera Sugar ambayo inaonekana kusuasua msimu huu kwani wapo katika hali ya kushuka daraja.
Kagera Sugar.
Katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga Vibonde wa ligi hiyo timu ya Coast Union watacheza na timu ya JKT Ruvu huu mchezo utakuwa muhimu mno kwa wagosi wa kaya kama wakifungwa ama kutoka sare ndo safari yao ya kushuka daraja itakuwa mwisho kushiriki ligi kuu msimu ujao.
Simba.
Siku ya Jumapili kutakuwa na mchezo moja utakaochezwa katika uwanja wa taifa kucheza na vijana wa Mwanza Toto Africa wekundu wa msimbazi Simba wanataka kuendeleza ubabe kwa Toto ili waweze kuendelea kufukuzia ubingwa msimu huu.
Toto Africa.

 Powered by Blogger.