Tazama Jinsi Atletico Madrid Ilivyoibamiza Bayern Munich UEFA Champion League.

Baadhi ya wachezaji wa Madrid wakishangilia.
Michuano ya kombe la klabu Bingwa barani Ulaya -Uefa Championi ligi- hatua ya Nusu fainali imeendelea tena jana.
Wakicheza katika dimba la Vicent  Atletico Madrid waliwakaribisha Bayern Munich toka Ujerumani katika mchezo wa pili wa nusu fainali baada ya mechi ya Man City na Real Madrid kuchezwa.

Timu ya Atletico Madrid imefanikiwa kuchomoza na ushindi katika mchezo huo kwa bao 1-0 bao lililofungwa na Saul Niguez dakika ya 11 na likiwa ni bao pekee katika ushindi dhidi ya Bayern Munich.
Saul Niguez.
Timu hizo zitarudiana tena wiki ijayo ikiwa ni mchezo wa mwisho kuweza kumpata mshindi atakaye cheza hatua ya Fainali ya michuano hiyo itakayofanyika nchini Italia mwezi wa tano.
Powered by Blogger.