Simba Yapokea Kichapo Toka Kwa Toto Africa,Huku Mashabiki Wamzomea Hans Pope Soma Hapa.

Simba.

Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara iliendelea jana kwa mchezo mmoja kupigwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam wakicheza ugenini timu ya Toto Africans, wamewazuia wekundu wa Msimbazi Simba Sport klabu kurejea kileleni mwa ligi kuu Tanzania baada ya kupokea kichapo cha bao 1-0.
 Wakicheza kwa nidhamu na kwa utulivu Toto Africa walipeleka  simanzi Msimbazi Dakika ya 20 ya mchezo bao hilo likifungwa na mchezaji Waziri Shentembo Junior kwa Shuti kali lililopigwa toka umbali wa Mita 25.

Katika mchezo huu Kocha wa Simba Jackson Mayanja alipewa kadi nyekundu baada ya kumtolea maneno machafu mshika kibendera, na beki mahiri wa kikosi hicho Hassan Kessy walilabwa kadi nyekundu kwa kumchezea vibaya mshambuliaji wa Toto Edward Christopher huku Simba wakionekana kuutawala mchezo huu walishindwa kabisa kupata bao licha ya kupata nafasi za wazi .

Kwa Matokeo haya yamewaacha Simba Nafasi ya 2 wakiwa na pointi 57 kwa michezo 25 huku Yanga wakiwa kileleni wakiwa na pointi 59 kwa michezo 24. Huku Azam Fc wapo nafasi ya 3 wakiwa na pointi 55 kwa mechi 24.
Mwenyekiti wa usajili Simba Zakaria Hans Pope.
 Mwenyekiti wa usajili wa klabu hiyo Zakaria Hans Pope alipata wakati mgumu kwa mashabiki baada ya kuanza kumzomea na kumshambulia kwa maneno mpaka kupelekea kutolewa nje kwa ulinzi mkali huku sauti za mashabiki hao wakisema viongozi wanaihujumu timu kutokana na kuwa bize na pesa za Emmanueli Okwi.

Powered by Blogger.