Siku Chache Baada Ya Roma Kuoa, Ndoa Yake Yaanza Kuchokonolewa.


MKALI WA Hip Hop Bongo, Ibrahim Mussa ‘Roma Mkatoliki’ ambaye siku chache zilizopita aliaga ubachela na kumuoa mwandani wake wa siku nyingi aitwaye Nancy, ndoa yake imeanza kuchokonolewa kwa kuibuliwa madai ya jamaa huyo katelekeza watoto.
Sekeseke hilo liliibuka baada ya picha zake za harusi kuzagaa mtandaoni ndipo ukazuka uvumi kuwa kuna watoto Roma kawatelekeza hivyo anapaswa kuwapa matunzo na kumuweka wazi mkewe ili kuinusuru ndoa yake.
Roma alipovutiwa waya na paparazi na kuulizwa juu ya madai hayo ya kuwatosa wanaye wa nje alisema:
“Kwanza hiyo ishu ndo’ naisikia kwako, halafu sipendagi sana kufuatilia mambo. Waache waongee wakichoka watanyamaza, huo ni uzushi mtupu, najivunia maisha ya ndoa,”


Chanzo:Gazeti La Ijumaa
Powered by Blogger.