Mshindi Wa Urais Nchini Djibouti Atangazwa

Serikali ya Djibouti imesema kuwa rais Ismael Omar Guelleh, amechaguliwa tena kwa muhula wa nne kama rais.
Akiongoa kwenye runinga ya taifa nchini humo, waziri mkuu wa nchi hiyo Abdoulkader Kamil Mohamed amesema Guelleh , ambaye alitwaa madaraka ya nchi hiyo mwaka wa tisini na tisa atashinda kura hiyo moja kwa moja kufuatia uchaguzi uliofanyika siku ya Ijumaa.
Vyama vitatu vya upinzani vilisusia uchaguzi huo.
Mashirika ya kutetea haki za kibinaadamu yamemshutumu bwana Guelleh kwa kudhibiti uhuru wa kimsingi nchini humo.
Nafasi ya Djibouti katika eneo la bahari ya shamu, limeipa nafasi muhimu duniani.
Taifa hilo ndilo la pekee barani Afrika ambalo lina kambi ya kudumu ya wanajeshi wa Marekani


 Published By: Frank Pande (@EnkyBanks Unaweza Kuzipata Story Zote Za Ndani Na Nje Ya Bongo Kwa Kujiunga Na SeetheAfricanLink Kwenye: Facebook|Twitter|Instagram|YouTube|Audiomack
Powered by Blogger.