Maamuzi Ya UEFA Baada Ya Kugundulika Sakho Alitumia Madawa
 Beki wa Liverpool Mamadou Sakho anachunguzwa na UEFA kwa kufeli ukaguzi wa madawa ya kulevya.
Ijapokuwa raia huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 26 hajapigwa marufuku rasmi, hatashiriki mechi yoyote wakati uchunguzi huo unapoendelea kulingana na Liverpool.
BBC radio 5 inasema kuwa Sakho alipatikana na dawa za kusisimua misuli baada ya mechi ya UEFA kati ya Liverpool dhidi ya Manchester United.
Sakho aliyesajiliwa kwa pauni milioni 18 kutoka Paris St-Germain mwaka 2013 amecheza mechi 34 msimu huu ikiwemo mechi 10 katika ligi ya Yuropa.
Alifunga katika ushindi wa Liverpool wa 4-3 dhidi ya Borussia Dormund mnamo tarehe 14 mwezi Aprili na kufuzu katika nusu fainali ya kombe hilo.

Powered by Blogger.