Ratiba Ya Ligi Ya Uingereza Ipo Hapa Ni Vita Ya West Ham Na Arsenal.

Wachezaji wa Arsenal na West Ham.

Ligi Kuu ya Uingereza kuendelea tena wikendi hii nyasi za viwanja saba zitawaka moto katika mshike mshike huu. 

Timu ya West Ham wagonga  nyundo wa London , watakua wenye wa washika bunduki wa London  Arsenal,huku  Aston Villa wanaoburuza mkia watakua nyumabni Villa Park kuwakabili Bournemouth.

Matajiri wa Man City watashukuka katika uwanja wao wa Etihad kusaka alama tatu kwa kucheza na West Bromwich Albion, Huku Swansea wakikipiga na Chelsea mchezo utaochezwa katika dimba la Libert.
Michezo mingine Crystal Palece watacheza na Norwich City,Southampton watawaalika vibonde wa Benitezi timu ya Newcastle na Watford baada ya kupokea kichapo cha mabao 4-0 toka kwa Arsenal wakuwa wenyeji dhidi ya Everton ambao nao walipokea kichapo cha 1-0 kutoka kwa Man United.
 
Michezo hiyo itaendelea siku ya Jumapili mechi tatu kuchezwa vinara wa Ligi hiyo timu ya Leceister City watakuwa ugenini kucheza na vibonde Sunderland,huku katika uwanja wa Tottenham baada ya kutoka sare ya 1-1 na Liverpool,Spurs watakuwa nyumbani kucheza na mashetani wekundu Man United na Liverpool watakuwa nyumbani kucheza na Stoke City.

  Published By: Alex Sonna. UnawezaKuzipata Story Zote Za Ndani Na Nje Ya Bongo Kwa Kujiunga Na SeetheAfricanLinkKwenye:Facebook|Twitter|Instagram|YouTube|Audiomack
Powered by Blogger.