Rais Shein Wa Zanzibar Atangaza Baraza La Wawakilishi.Hatimaye Rais wa Serikali ya Mapunduzi ya Zanzibar ametangaza Baraza lake lawawakilishi akiwemo Hamad Rashid kutoka Chama cha Upinzani cha ADC.
Hamad Rashid Mohamed aliwahi kuwa mwanachama machachari wa Chama cha Upinzani, CUF kilichosusia uchaguzi wa marudio kwa madai kuwa kiliporwa ushindi katika uchaguzi wa awali uliofanyika mwezi Oktoba mwaka 2015.
Hamad Rashid alifukuzwa katika CUF akagombea Urais kwa Tiketi ya Chama cha Alliance for Democratic Change na kuambulia nafasi ya pili.
Hata hivyo hakufikia asilimia 10 ya kura zote ili apate nafasi ya kuwa makamu wa kwanza wa rais kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar iliyopatikana baada ya mvutano mkubwa kati ya Chama cha CUF na CCM.
Hii ndio Orodha ya baraza hilo la wawakilishi:
Powered by Blogger.