Pesa Ya Zambia Yafanya Vizuri Duniani Na Hizi Ndo Sababu Zake Zijue?

Dola.
Sarafu ya Zambia ya Kwacha ndiyo sarafu iliyo na biashara nzuri zaidi duniani mwaka 2016, kwa mujibu wa shirika la habari la Bloomberg.
Shirika hilo linasema kuwa thamani yake dhidi ya dola ya marekani imepanda kwa asilimia 19.9 tangu mwezi Januari.
Hii inajiri baada ya sarafu hiyo kuorodheshwa kwa kuwa moja ya sarafu zilizokuwa na biashara duni zaidi duniani mwaka uliopita.
Hali hii ilitokana na kushuka kwa bei ya shaba nyekundu ambayo ndiyo moja ya bidhaa muhimu inayouzwa nje pamoja na kuwepo uhaba wa nishati.
Bloomberg imenukuu wadadisi wakisema kuwa sarafu ya Kwacha itazidi kuboreka wakati bei ya shaba inaimarika.
Powered by Blogger.