Nyange Kaburu Kuamua Kesi Ya Coast Union Na Yanga Kesho Nani Atamfuata Azam Fainali Ya FA.

Nyange Kaburu.
 Kamati ya TFF inatarajia kukaa na kutoa hatima ya mchezo kati ya Coast Union ya Tanga na Yanga,kesi hiyo itasikilizwa kesho ikiongozwa na makamu wa Rais wa Simba Geodfrey Nyange Kaburu ambaye ni mwenyekiti wa kamati hiyo ya mashindano hayo.
Mechi kati ya Coastal Union na Yanga ilievunjika baada ya kuchezwa Dakika 15 tu za Dakika za Nyongeza 30 huku Yanga wakiongoza 2-1.
 Coastal walitangulia kufunga kwa Bao la Dakika ya 55 la Yusuph Sabo na Donald Ngoma kuisawazishia Yanga katika Dakika ya 61.
Bao hizo zilibaki hadi Dakika 90 zinakwisha na kuongezwa Dakika za Nyongeza 30 na yanga kufanikiwa kuandika Bao lao la Pili Dakika ya 95 Mfungaji akiwa Amisi Tambwe.
Dakika ya 101, Coastal walibaki pungufu kwa kucheza 10 baada ya Adeyum Ahmed kupewa Kadi ya Njano ya Pili na kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu.
Hadi Dakika 15 za kwanza kumalizika, Yanga walikuwa mbele kwa Bao 2-1 lakini Mechi hiyo ilivunjika kutokana na vurugu za Mashabiki huku pia giza likishamiri Uwanjani.
Hivyo ripoti ya kutoka kwa kamisaa wa mchezo pamoja na kamati ya mashindano itatoa majibu sahii kuhusiana na mchezo huo siku ya kesho.
Powered by Blogger.