Ni Vita,Ubabe Na Kisasi Atletico Madrid Na Barcelona Huku Bayern Munich Ugenini UEFA Champions League.

Michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya inaendelea leo katika hatua ya robo fainali viwanja viwili vitani kutafuta timu mbili zitakazofuzu hatua ya nusu fainali na kuungana na Man City na Real Madrid zilizofuzu jana.
Uwanja wa Estadio Vicent Calderon.
Katika uwanja wa Estadio Vicent Calderon kutakuwa na shughuli pevu pale timu ya Atletico Madrid watakuwa wenyeji wa Barcelona mchezo huu utakuwa na upinzani kutokana na mechi ya kwanza Atletico Madrid walifungwa mabao 2-1 mabao yakifungwa na Louis Suarez aliyefunga mawili na Torres akifunga bao moja.
Philipe na Suarez.
Mchezo huu ni mgumu endapo wenyeji watapata bao moja watafuzu moja kwa moja kutokana na kuwa na bao moja la ugenini na Barcelona wanasaka rekodi ya kuchukua ubingwa mara mbili kwa mfululizo.
Atletico Madrid.
Nchini Ureno katika uwanja wa Estadio Da Luz wenyeji wa mchezo huo Benfica watawakaribisha Bayern Munich kutoka Ujerumani hii nayo itakuwa ngumu kutokana na mechi ya awali wajerumani walishinda bao 1-0.
Bayern Munich.
Benfica wataingia kwa kusaka ushindi ili waweze kuingia hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo kutokana na kufungwa ugenini walipocheza nchini Ujerumani.
Benfica.
Michezo hizo zitakamilika na kufanya kuwa timu nne ambazo zitakuwa zimeingia hatua ya nusu fainali na droo itapangwa Ijumaa ili kujua nani atkutana na mwenzie.


Powered by Blogger.